Benin watua Dar tayari kuwavaa Stars Jumapili hii
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.