Sarafu mpya kuanza kutumika Oktoba Mosi
Benki Kuu ya Tanzania imesisitiza kuwa sarafu mpya ya shilingi mia tano itaanza kutumika Oktoba Mosi mwaka huu kama ilivyopangwa hapo awali, sambamba na pesa ya noti kwa ajili ya manunuzi yote yenye thamani ya shilingi mia tano.