Wahariri waja juu sakata la kupigwa waandishi
Jukwaa la wahariri nchini Tanzania limesema litamwandikia barua mkuu wa jeshi la polisi IGP Ernest Mangu kutaka askari wote walioshiriki kuwapiga hadi kuwajeruhi waandishi wa habari hapo jana kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.