Ruto akiri mauaji ya wanawake yamezidi Kenya
Rais wa Kenya William Ruto, amekiri kuwepo kwa changamoto kubwa ya mauaji nchini kwake kufuatia mfululizo wa visa vya mauaji hasa ya wanawake na wasichana nchini humo, huku akisema kwamba kama Taifa inabidi suala la uhalifu na maadili liangaliwe kwa upana zaidi.