Yanga yapoteza mchezo wa kwanza msimu 2024-2025

Kikosi cha Wanajangwani kimesalia na alama zake 24 bado kikiwa kinaongoza msimamao wa ligi kuu Tanzania bara, Singida Black Stars inashika nafasi ya ya pili ikiwa na alama 23 na Simba SC yenye alama 22 ipo nafasi ya 3 baada ya timu za Kariakoo kucheza michezo 9 kila moja Singida Black Stars imecheza michezo kumi ya ligi mpaka sasa.
Klabu ya Yanga jana imepoteza kwa mara ya kwanza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam SC huo mchezo uliochezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam. Goli la Wahoka Mikate tokea Chamazi liliwekwa kimiani na nyota wa kimataifa wa Gambia Gibril Sillah.