Majeruhi Yanga SC yampa mtihani Gamondi

Kesho Novemba 2 Yanga itakuwa uwanjani kukabiliana na Azam FC kwenye muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara kuna wasiwasi timu hiyo ikacheza mchezo huo bila Mabeki wa pembeni Yao Kuoassi na Shedrack Boka ambao ni majeruhi Nickson Kibabage naye akiwa hatihati kutokana na kupata maoumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars.
Kocha wa Yanga Miguel Gamondi anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha Yanga SC kutokana na ugumu wa ratiba ya Yanga SC kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara huku kikosi chake kikiwa na Wachezaji majeruhi ambao muhimu kwake kulingana na aina ya uchezaji wa timu hiyo.