Askofu awasihi UKAWA kurejea bungeni
Askofu mstaafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri nchini Tanzania, Elinaza Sendoro, amewaonya wafuasi wa UKAWA katika Bunge Maalumu la Katiba kuacha misimamo inayotishia kukwamisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.