Maambukizi ya Malaria nchini Tanzania yapungua
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Dkt. Seif Rashid, amesema kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa Tanzania Bara kimepungua kwa takriban asilimia 50 kutoka asilimia 18 mwaka 2008 hadi asilimia 10 mwaka 2012.