Wizi wa mitandao bado ni changamoto - Serikali
Serikali ya Tanzania imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika sekta ya mawasiliano hasa suala la uhalifu wa kutumia mtandao na imeahidi kwamba hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu itakua imetunga sheria tatu zitakazosimamia tatizo hilo.