Ruben Amorim anatajwa kuwa Kocha mpya Man United

Kocha wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Ruben Amorim kwa mujibu wa vyombo vya Habari barani Ulaya vinamtaja kuwa ndiye kocha anayetizamiwa kuchukua nafasi ya Erik Ten Hag ndani ya Manchester United baada ya timu hiyo kutangaza kumfuta kazi Kocha huyo raia wa Uholanzi siku ya jana. Klabu ya Man United na Sporting Lisbon zipo kwenye majadiliano juu ya uhamisho wa Kocha huyo bora kwa sasa nchini Ureno.
Kocha huyo anayefundisha Sporting Lisbon ambayo ni Mabingwa watetezi wa ligi ya Ureno na ndiyo vinara wa ligi hiyo msimu huu wa 20245-2025 ikiwa na alama 27, katika michezo tisa ikifunga goli 30 na kuruhusu goli mbili .