Ten Hag afutwa kazi Manchester United

Klabu ya Manchester United ya Uingereza imetangaza kumfuta kazi kocha wake Erik Ten Hag. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Ten Hag amepata taarifa ya kufutwa kwake kazi asubuhi ya leo baada ya jana kupoteza mchezo wa ligi kuu Uingereza ugenini uwanja wa London Stadium nyumbani kwa timu ya West Ham United.

Kocha huyo raia wa Uholanzi alijiunga na Man United mwaka 2021 akitokea timu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi. Amekiongoza kikosi cha Mashetani Wekundu kushinda ubingwa wa  FA msimu uliopita 2023-2024 na kombe la ligi ( EFL) 2022-2023.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS