Rekodi zinaibeba Madrid kuelekea El Clasico

Mabingwa watetezi wa La Liga mara ya mwisho kupoteza mchezo wa ligi ilikuwa miezi 13 iliyopita na imecheza michezo 42 bila kupoteza, Barca inashakilia rekodi za kutokupoteza kwenye michezo 43 ya ligi  iliyoanzia 2017 na 2018.Michezo mitatu iliyocheza Madrid dhidi ya Barcelona hivi karibuni  kikosi cha Carlo Ancelotti kimeshinda michezo yote.

Kuelekea mchezo wa El Clasico utakaochezwa kesho Jumamosi  Oktoba 26, 2024 rekodi zinaibeba Real Madrid mbele ya Wapinzani wao kutoka Jimbo la Catalunya FC Barcelona na timu hiyo Mabingwa watetezi wa ligi kuu Hispania inatarajiwa kuweka historia kwenye mchezo huo.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS