Mashabiki Simba kuchangia damu Okt,16
Mfadhili wa zamani wa klabu ya Simba, Azim Dewji amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze siku ya Jumamosi kuchangia damu ikiwa kama sehemu ya sadaka katika mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Premio De Agosto utaopigwa jumapili hii katika dimba la Benjamin Mkapa.