Trent Alexander- Arnold aipasua kichwa Liverpool

Trent- Alexander Arnold amegomea mkataba mpya wa kusalia kikosi cha Liverpool na kuamsha presha kwa Mabosi wa klabu hiyo juu ya mustabali wa mchezaji huyo ndani ya timu hiyo. Taarifa zinazowastua zaidi Uongozi wa Majogoo wa Jiji ni kuhusiana na jina la nyota huyo kuwepo kwenye listi ya Wachezaji wanaohitajika kwenye kikosi cha Real Madrid ya Hispania dirisha kubwa usajli mwezi Julai 2025.
Mkataba wa Trent ndani ya Liverool unatamatika mwishoni mwa msimu wa 2024-2025.
Trent - Alexander Arnold raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na klabu ya Liverpool mwaka 2004, alipanda kucheza kikosi cha wakubwa mwaka 2016 amekitumikia kikosi cha Majogoo ya Jiji la Anfield kwa mafanikio ameshinda kombe la ligi kuu Uingereza na Klabu bingwa barani Ulaya.