Machinga wayakimbia masoko rasmi Mwanza
Baadhi ya masoko yaliyotengwa yatumike na wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga katika manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametajwa kutelekezwa na wafanyabiashara hao na kurejea tena kuendesha biashara zao maeneo yasiyo rasmi ya pembezoni mwa barabara ambayo yanatishia usalama wao.