Fred Minziro aitwa kuokoa Jahazi la Pamba FC

Fred Felix Minziro amejiunga na timu ya Pamba ya Jijini Mwanza baada ya timu hiyo kumfuta kazi Goran Kopunovic. Pamba imeshacheza michezo saba ya ligi kuu Tanzani bara msimu huu wa 2024-2025 mpaka sasa, imetoka sare michezo minne na kupoteza michezo mitatu na inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 4.
Minziro kocha mwenye uzoefu mkubwa wa kufundisha mpira wa Tanzania baada ya kufundisha timu mbalimbali nchini Tanzania. Katarai Majeshi Baba Isaya aliiongoza timu ya Geita Gold FC kumaliza nafasi ya nne ambayo iliipa timu hiyo nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho barani Afrika.