Shirika la Posta lawasaidia watoto mkoani Rukwa
Shirika la Posta Tanzania Sumbawanga Mkoani Rukwa, limetoa msaada wa wa vyakula na mafuta kwa watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma shule ya Msingi Malamngali, inayohudumia watoto wenye mahitaji maalum ikiwa ni juhudi za kuhakikisha wanapata huduma stahiki na afya bora.