Walioshinda 'Golden Buzzer' wamshukuru Rais Samia
Vijana wawili wanaojiita za The Ramadhan Brothers, ambao video yao ilisambaa mitandaoni wakiwa kwenye mashindano ya Australia got talent, na kubonyezewa Golden Buzzer baada ya kufanya mazuri wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa namna ambavyo imekuwa ikiwatia moyo wasanii.