Wananchi waangua kilio kuondolewa wanapoishi
Zaidi ya wakazi 7000 wanaoishi eneo la Bondo, Kata ya Kwamagome Handeni mkoani Tanga, wamekumbwa na taharuki baada ya kutakiwa kuondoka kwenye eneo wanaloishi kwa zaidi ya miaka 40 na waende kusikojulikana kupisha eneo hilo linalodaiwa kuwa ni mali ya wakala wa Huduma za Misitu (TFS).