Umeme wa jua wateketeza nyumba
Simanzi na vilio vimetawala kwenye familia ya Lenard Ramadhani na Happyness Richard, wakazi wa mtaa wa Tulieni, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto huku chanzo kikitajwa kuwa ni umeme wa jua na kuokoa pikipiki na sofa seti moja pekee.