Waziri Mabula aagiza upembuzi wa mashauri ya ardhi

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili Kulia) pamoja na Katibu Mkuu Dkt Allan Kijazi (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara wakiwasili kwenye kikao kazi baina ya Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza ufanyike upembuzi wa mashauri yote ya ardhi yaliyokaa muda mrefu kutokana na sababu zisizo na mashiko.