WATAKAOTOROSHA MADINI WANAITAFUTA JELA
Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko amewaonya wachimbaji wa Dhahabu wanaotorosha madini hayo kwa kupunguza thamani yake kukiona cha moto kwani serikali imejenga miundombinu ya kuuzia dhahabu na imepunguza gharama ya tozo zilizokuwa zinawafanya wachimbaji wakwepe masoko ya ndani.