Waziri Mabula atoa maelekezo kwa watendaji
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kujipanga na kufanya kazi kwa pamoja na wataalamu wa ardhi ili kuondoa changamoto zinazojitokeza katika utendaji kazi na usimamizi wa sekta ya ardhi katika Halmashauri.