Mapinduzi yanukia Burkina Faso
Kunasikika milio mikubwa ya risasi nchini Burkina Faso katika mji mkuu Ouagadougou huku kukiwa na taarifa kwamba Televisheni ya Taifa imezimwa. Baadhi ya barabara zimefungwa kwenye mji huo mkuu huku mitandao ya kijamii ikisema kwamba huenda kuna mapinduzi yanafanyika.