Rodri ashinda tuzo ya BALLON D'OR

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 majina ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo yamekosekana kwenye orodha ya tuzo hizo. Zaidi ya miaka kumi na tano tuzo hizo zilitawaliwa na Wachezaji ambao wanatajwa kama Wachezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea Duniani Messi na Ronaldo.

Nyota wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Hispania Rodrigo Hernández Cascante, maarufu kama Rodri ameshinda tuzo ya Ballon D'or  kwenye sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika Jiji la Paris nchini Ufaransa. Rodri ameshinda tuzo hiyo mbele ya Vinicius Junior wa Real Madrid

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS