Mama achoma mikono ya bintiye wa darasa la 7
Helena Mashaka (13), mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Shahende iliyopo Kata ya Butobela, mkoani Geita, amechomwa mikono yake kwa moto na Mama yake kwa tuhuma za kuiba shilingi 30,000 na kupelekea mwanafunzi huyo kushindwa kufanya mitihani yake ya kuhitimu.


