Eric Cantona aucharukia Uongozi wa Man United

Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United ameujia juu Uongozi wa Manchester United baada ya Mabosi wa klabu hiyo kumuondoa Sir Alex Ferguson kwenye nafasi yake ya Ubalozi wa Mashetani Wekundu wa Jiji la Manchester. Ferguson Kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Mameneja wa Kingereza, aliiongoza Man U kushinda makombe 13 ya ligi kuu Uingereza, Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili na Kombe la klabu bingwa Dunia msimu wa 2007-2008. Cantona alikuwa Mchezaji muhimu alitoa mchango mkubwa kwenye klabu ya Manchester United alishinda makombe ya ligi EPL mara 4 katika miaka 5.

Sir Alex Ferguson ameiongoza Manchester United kwa miaka 26, Aliiongoza klabu hiyo yenye makazi yake Old Trafford kushinda mataji 38 kwa ujumla. EPL Makombe 13, FA Makombe 5 sambamba na kombe la ligi ya mabingwa mara 2. Kocha huyo raia wa Scotland aliiongoza United tangu mwaka 1986-2013.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS