Unafuu wa tozo kwa wananchi waja
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Wizara ya Fedha na Mipango, imepokea maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi (CCM),kuhusu kushughulikia malalamiko ya wananchi yaliyojitokeza kuhusu gharama za tozo za miamala ya kielektroniki ili kuleta unafuu wa wananchi.