Tanzania yalegeza masharti ya UVIKO, 808 wafariki
Serikali imetangaza kulegeza masharti ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19, ambapo kuanzia sasa hakutakuwa na ulazima wa kuvaa barakoa isipokuwa kwa mtu mwenye mafua pale itakapomlazimu sambamba na kwenye misongamano ya watu.