Caroline Garcia afuzu nusu fainali US Open
Mcheza tennis raia wa Ufaransa Caroline Garcia amefuzu kwa mara ya kwanza kucheza hatua ya nusu fainali kwenye tennis. Hii ni mara baada ya kumfunga Coco Gauff raia wa Marekani kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya wazi ya Marekani (US Open).