"Mikopo ya elimu haitolewi kwa undugu" - Waziri
Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda, amesema kuwa serikali haiwezi kutoa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa undugu, urafiki ama kwa kujuana kwani shughuli za elimu zinahitajika kwa kila mtu na hivyo ni wajibu wa serikali kufanya kwa haki na uwajibikaji uliotukuka.