Wananchi watakiwa kusalimisha silaha kwa hiari
Wananchi wametakiwa kujitokeza katika kampeni maalum ya mwezi wa msamaha wa Afrika itakayohusisha usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari katika vituo vya polisi, ofisi za Serikali za mitaa, ofisi za watendaji wa Serikali za mitaa na vijiji.