Mazingira ya uwekezaji ni mazuri - Waziri Ndaki
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza katika sekta ya mifugo huku akisisitiza kuwa mazingira ya uwekezaji kwa sasa hapa nchini ni salama chini ya Uongozi wa Rais wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.