Chalamila aagiza taasisi zinazodaiwa zikatiwe maji
Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila, ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), kusitisha huduma kwa taasisi za serikali ambazo zimelimbikiza madeni kwa kushindwa kulipa ankara za maji kwa wakati, na kusababisha mamlaka hiyo kushindwa kujiendesha.