Tanzania haijafanya kosa lolote - Balozi Kombo
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi msimamo wake kuhusu hali ya kisiasa nchini, ikisisitiza kuwa hakuna sheria yoyote iliyovunjwa katika utekelezaji wa majukumu yake kama taifa huru linalozingatia utawala wa sheria.