Basi la Tanzanite laua watano Singida
Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya basi la kampuni ya Tanzanite imeongezeka kutoka vifo vinne hadi vitano hii leo. basi hilo lilipata ajali jana Agosti 17, 2022, katika Kijiji cha Mbwasa wilayani Manyoni mkoani Singida wakati likitoka jijini Mwanza kuelekea Dar es Salaam.