Uchunguzi miili iliyokutwa kwenye viroba - Masauni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni ameagiza kufanywa uchunguzi wa kina ili kubaini mauaji ya kinyama dhidi ya watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wachimbaji wa madini ambao miili yao ilikutwa kwenye viroba na kutupwa kwenye kijiji cha Lusane kata ya Tunguli Mkoani Tanga