Chicharito kurejea Manchester United?
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez “Chicharito” ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani amesema yupo tayari kurejea Manchester United ili kusaidi kutatua changamoto ya eneo la ushambuliaji ambalo linaonekeana kuisumbua klabu hiyo kwa sasa.