Polisi waongezewa nguvu kupambana na panya road
Jeshi la Polisi nchini limeongezewa nguvu na makampuni binafsi ya ulinzi ili kuzuia uhalifu wa panya road ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo makampuni hayo yameahidi kutoa magari 8, pikipiki 3, askari na mafuta yenye thamani ya Tsh 350,000, ili kusaidia katika doria mbalimbali.

