Haaland kafunga tena, Man City wanaongoza Ligi
Mabingwa wa England Manchester City wamepanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England EPL, baada ya kuinyuka Wolverhampton Wanderers mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Molineux. Sasa wanaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 2 dhidi ya Arsenal wanaoshika nafasi ya pili.

