Gari lamvamia bodaboda Dar es Salaam
Gari aina ya Harrier lenye namba T 210 DRC, limepata ajali baada ya kumvamia bodaboda aliyekuwa amepaki pembeni katika makutano ya barabara ya ITV jijini Dar es Salaam, na kusababisha uharibifu wa vyombo hivyo vya moto.