Joshua akubali Masharti ya Tyson Fury
Promota wa bondia Mwingereza Anthony Joshua Eddie Hearn amesema haoni kama kuna vizingiti vitakavyo sababisha pambano la uzito wa juu kati ya Anthony Joshua na Tyson Fury kutofanyika, amesisitiza kuwa Joshua anataka pambano lifanyike.

