Wafanyabiashara soko la Magomeni wapangwa upya
Baada ya wafanyabiashara katika Soko la Kimataifa la Magomeni kukimbia vizimba na maduka yaliyopo sehemu za juu na kwenda kufanyia biashara chini, sasa wamerejea katika maeneo yao ya ghorofani baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuunda kamati ya kuwapanga upya.

