Jela miaka sita kwa kosa la kujaribu kubaka
David Juma maarufu kama Kajeri mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Songe Manispaa ya Musoma mkoani Mara ambaye ni dereva wa pikipiki amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na kulipa faini ya shilingi Milioni 2.5 kwa kosa la kujaribu kubaka na kudhuru mwili wa binti wa miaka 26