"Bei ya mahindi yapanda mara mbili" - BoT
Wakati raia wakiendelea kulalama juu ya kupanda kwa bei ya nafaka, wakulima na wafanyabiashara huenda wakawa miongoni mwa watu walionufaika zaidi na zao la mahindi baada ya bei ya jumla ya zao hilo kupanda zaidi ya mara mbili ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

