Treni ya umeme Dar hadi Morogoro kuanza rasmi 2023
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amesema kwamba Treni ya umeme kutoka Dar es Salaam, hadi Morogoro itaanza kufanya kazi rasmi mwezi Februari 2023, kwani vichwa vya Treni, mabehewa ya abiria na mizigo yanatarajiwa kufika nchini mwezi Novemba.

