Mkongo wapigwa marufuku, una Viagra
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limepiga marufuku matumizi ya dawa aina ya Hensha maarufu kama Mkongo kwa binadamu, na kwamba tayari limekwishaifutia usajili baada ya kubaini imechanganywa na dawa za kuongeza nguvu za kiume (Viagra).