TAVA yaridhishwa na viwango ligi ya Taifa Wavu
Vilabu 20 kutoka mikoa 7 vinaendelea kuchuana vikali kugombania Taji la Ligi ya Taifa ya mchezo wa mpira wa Wavu 2022 inayoendelea kushika kasi kwenye uwanja wa ndani wa Taifa huku michezo ya mzunguko wa pili ikitaraji kuhitimishwa Septemba 24, 2022 jijini Dar es Salaam.

