"Vijana wengi warudi vijijini kulima"- RC Sendiga
RC Rukwa Queen Sendiga, amesema anatamani kuona mkoa wa Rukwa ukifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kiwe cha kibiashara na kukuza uchumi wa wananchi na kuwataka wataalam wa kilimo kuja na mikakati ya kufanya kilimo kikuze pato la wananchi na kuongeza uhakika wa chakula.