Dkt. Nchemba aahidi maji kwa wananchi wa Iramba
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewahakikishia wakazi wa Kata za Mgongo na Shelui Wilayani Iramba mkoani Singida, kwamba wataondokana na changamoto ya uhaba wa maji hivi karibuni kupitia mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria.